Lyrics
[INTRO – Lonely Blues Guitar | Spoken/Sung Softly]
Ohhh… Fidelis Faith…
Umeondoka umeniacha mpweke…
Nikijiuliza moyoni mwangu…
Kwa nini uliondoka?
Kwa nini uliniacha…
Nikiwa bado nakupenda?
Fidelis Faith…
---
[VERSE 1 – Slow, Painful]
Fidelis Faith…
Nilikuupa moyo wangu wote,
Ambao haukugawanyika.
Nilikuamini hata nilipoonywa…
Kwa tofauti za kabila zetu.
Kwa imani moja yetu ya Ukristo,
Nikakuchagua wewe…
Kabla sijajichagua mimi.
Fidelis…
Sikukuona kama mke tu…
Nilikuona wewe ni maisha yangu yote.
Fidelis…
Lakini siku moja ukabadilika…
Ukaondoka kimya kimya…
Ukaniacha na upweke…
Na upendo ambao
Haukuwa na pa kwenda.
Fidelis…
---
[PRE-CHORUS – Emotional Build]
Nilikuomba ubaki…
Moyo wangu ukakulilia…
Lakini macho yako hayakuona
Machozi yaliyokuwa yakinitoka.
Wala masikio yako…
Hayakusikia kilio changu…
Sikujua mtu unayempenda…
Anaweza kuwa sababu ya kulia…
Kila siku.
Fidelis…
---
[CHORUS – Heartbreaking | Strong but Slow]
Fidelis Faith…
Uliniacha nikiwa bado nakupenda.
Fidelis Faith…
Ukaondoka…
Moyo wangu ukiwa mikononi mwako.
Fidelis Faith…
Nimebaki na picha zako…
Nimebaki na sauti yako kichwani…
Nimebaki na maswali yasiyo na majibu…
Fidelis Faith…
Kwa nini uliondoka…
Wakati nilikuwa bado nakuhitaji?
Fidelis Faith…
Nikiwa bado nakupenda…
---
[VERSE 2 – Memories | Guitar Lead]
Fidelis…
Nakumbuka tulipokutana mara ya kwanza…
Ulipokuwa COTC Mtwara.
Ulijitambulisha kama Faith…
Nami nilizoea kukuita Faith…
Na hata ulipokuwa ukija Mashujaa…
Tulipokuwa tukikutana…
Muda ule nikiwa Mtwara…
Yote bado nayakumbuka…
Fidelis...
Tulipokutana kwa mara ya kwanza…
Moyo ulikupenda…
Japo haikuwa rahisi.
Lakini ulitambua…
Nimekupenda, Fidelis…
Nilifumba macho yangu…
Sikuwaona wanawake wengine…
Nilijua nimekupata…
Mke wa ndoto zangu.
---
[SUB-CHORUS – Crying Tone]
Fidelis Faith…
Mbona nilikupenda?
Fidelis Faith…
Mbona nilikuamini?
Fidelis Faith…
Mbona nilikuthamini?
Nilijua utabaki…
Nilijua utanipenda…
Fidelis Faith…
---
[VERSE 3 – Deep Emotional]
Nilithamini uwepo wako…
Kwa kuitafuta furaha yako.
Nilijitahidi kujinyima…
Kwa lolote lililokupata.
Hata kama ilikuwa kidogo…
Nilitenda kwa upendo.
Sikufanya kwa kujionyesha…
Nilifanya kwa sababu nilikupenda.
Nilifungua moyo wangu wote…
Nikakupa kila kilichokuwa bora kwangu…
Hakuna nilichokuficha…
Hata ya sirini nilikupatia.
Ni wapi nilikosea, Fidelis?
Tafadhali…
Nijulishe, Fidelis…
---
[CHORUS – Emotional | More Pain]
Fidelis Faith…
Nimebaki na picha zako.
Fidelis Faith…
Nimebaki na sauti yako kichwani…
Nimebaki na maswali yasiyo na majibu…
Fidelis...
Kwa nini uliondoka…
Wakati nilikuwa bado nakuhitaji?
[Deep Lonely Melody]
Sikukupoteza kwa sababu sijui kupenda…
Najua uliondoka…
Sababu sikua chaguo kwako, hukunipenda.
Fidelis Faith…
Mimi bado nakupenda…
---
[VERSE 4 – Lonely Night | Very Soft]
Fidelis…
Leo umeondoka…
Nimebaki na upweke usio na mwisho…
Fidelis…
Kila nikiwasha simu…
Nakuta jina lako…
Natamani nikwambie…
“Nakumiss…”
Lakini ghafla nakumbuka…
Hauko na mimi tena.
Fidelis…
Kuna nyimbo nikizisikia…
Nakumbuka tulivyokuwa tukikutana Mashujaa.
Najaribu kupotezea…
Lakini nalazimishwa nikukumbuke…
Fidelis…
Leo nakuimbia kwa uchungu…
Tafadhali… rudi, Fidelis…
Utarudi kweli?
Utanipenda tena kweli?
Utajali hisia zangu?
Fidelis Faith…
Au ndiyo umeondoka…
Milele?
Fidelis?!
---
[PRE-BRIDGE – Almost Crying | Music Drops]
Fidelis Faith…
Najua upo mbali nami…
Najua hunikumbuki…
Lakini wimbo huu…
Uwe ukumbusho kwako.
Najua siku moja…
Maisha yangu yatakoma.
Kaburini nitatulia…
Lakini wimbo huu, Fidelis…
Kamwe hautanyamaza.
Kila muda utakukumbusha…
Jinsi nilivyokupenda.
Kila ukiusikia…
Jua tu, Fidelis…
Nilikupenda kwa kweli.
---
[BRIDGE – Very Soft | Almost Crying]
Fidelis Faith…
Natamani ujue…
Nilivyokupenda…
Fidelis Faith…
Natamani ujue…
Moyo wangu ulikupenda kwa kweli…
[Long instrumental pause]
Fidelis…
---
[FINAL CHORUS – Powerful & Painful]
Fidelis Faith…
Uliniacha nikiwa bado nakupenda.
Fidelis Faith…
Ukaacha moyo wangu ukiwa umevunjika.
Kama siku moja utanikumbuka…
Kumbuka nilikupenda kwa kweli.
Sikukupa moyo wangu kwa mchezo…
Nilikuona kama kesho yangu.
Lakini leo nimejifunza…
Si kila unayempenda…
Hubaki.
Fidelis Faith…
Ulienda na sehemu ya moyo wangu…
Na mimi nimebaki…
Nikijifunza kuishi…
Na maumivu haya.
---
[OUTRO – Lonely Blues Guitar | Voice Fading]
Ohhh… Fidelis Faith…
Bado nakukumbuka…
Bado jina lako linauma…
Uliniacha…
Nikiwa bado nakupenda…
Nikiwa bado nakuhitaji…
Fidelis…
Tafadhali rudi…
Bado ninakupenda…
Fidelis Faith…
Kuna siku hutaniona…
Wala hutonisikia…
Utatamani tukutane…
Hata kama useme tu…
“I'm sorry…”
Lakini utaliona kaburi…
Na picha zangu…
Ndipo utajua…
Nilivyokupenda.
Na labda siku hiyo…
Moyo wangu utakuwa umeacha kulia…
Fidelis Faith…
Ulini… acha…
Nikiwa bado…
Nakupenda…
[Guitar fades slowly]
Fidelis Faith…
Want to make R&B / Soul yourself? See how Star Singer compares to Suno and Udio for AI R&B / Soul generation.
Make a R&B / Soul like this with AI
Generate your own AI R&B / Soul song in 90 seconds — first one free, monetizable with a credit, vertical music video included.
FAQ
Who made "Fidelis Faith Bado nakuhitaji"?
"Fidelis Faith Bado nakuhitaji" was made by @silent_encore_97 on Star Singer, where anyone can write and sing an original song with AI.
What genre is Fidelis Faith Bado nakuhitaji?
Fidelis Faith Bado nakuhitaji is R&B / Soul.
Can I listen to "Fidelis Faith Bado nakuhitaji" for free?
Yes. "Fidelis Faith Bado nakuhitaji" streams free on Star Singer — no subscription required. You can also make your own: one AI song a day is free, extra songs with a lyric video are $1.99, a lip-synced music video starring you is $19.99, and cinematic videos start at $2.99.
Can I create my own AI song?
Yes. Star Singer lets you create AI-generated songs and music videos. Clone your voice, pick any style, and generate original music. Listening is free and unlimited, and one song a day is free to make — no subscription.
Thanks — this has been sent to our review team.