Lyrics
Mwanzo nilikuwa mtu wa tofauti,
Sikujua kukaa, nilikuwa na mengi yangu.
Lakini nilipokupenda, nikabadilika,
Nikawa mtulivu ili usiendelee kuumia.
Mwanzo na wewe tulikuwa sawa,
Ulinipa heshima, nami nikakupa moyo.
Niliona ndani yako mwanamke wa maisha yangu,
Nikaacha yale yaliyokuwa yanakuumiza.
Polepole ukaanza kubadilika,
Maneno yakawa makali, heshima ikapungua.
Nikakaa kimya kwa sababu nilikupenda,
Nikiamini bado yule mwanamke wangu yupo.
Anakosea namsamehe,
Analudia yaleyale.
Anakosea namsamehe,
Analudia yaleyale.
Nilivumilia kwa sababu nakupenda,
Nikanyamaza nisije nikakupoteza.
Lakini moyo nao una mwisho,
Na sasa umebaki na jeraha.
Sikuhitaji uwe mkamilifu,
Nilihitaji tu uniheshimu.
Maana mimi nilibadilika kwa ajili yako,
Ili usiendelee kuumia kwa sababu yangu.
Nilipoona kosa langu nilirekebisha,
Nilipoona nimekukwaza nikajifunza.
Lakini kwako makosa yakawa kawaida,
Na msamaha wangu ukawa kama ruhusa.
Bado nilikaa, bado nilipenda,
Kwa sababu moyo wangu haukujua kuacha.
Na sasa umeanza kuona nilichokuwa nakiona,
Machozi yako yameanza kunieleza.
Unasema unanipenda,
Unasema umebadilika.
Lakini nilipokuwa naumia,
Nilikuwa nikisubiri mabadiliko hayo.
Sasa mimi nimechoka,
Moyo wangu tayari umechoka.
Sio kwamba sikupendi,
Nilipenda mpaka nikajisahau.
Lakini nimeumia mara nyingi,
Mpaka mapenzi yakageuka jeraha.
Anakosea namsamehe,
Analudia yaleyale.
Nilisamehe mpaka nikachoka,
Nikapenda mpaka nikavunjika.
Sasa unanipenda,
Sasa unasema umebadilika.
Lakini moyo wangu umechoka,
Umechoka kuanza upya kila siku.
Mwanzo nilibadilika kwa ajili yako,
Leo umebadilika kwa ajili yangu.
Lakini moyo wangu umechoka.
Jeraha...
Want to make R&B / Soul yourself? See how Star Singer compares to Suno and Udio for AI R&B / Soul generation.
Make a R&B / Soul like this with AI
Generate your own AI R&B / Soul song in 60 seconds — first one free, full commercial rights, vertical music video included.
FAQ
Who is Unknown?
Unknown is an AI artist on Star Singer that produces R&B / Soul music.
What genre is My Song?
My Song is R&B / Soul.
Can I listen to "My Song" for free?
Yes. "My Song" streams free on Star Singer — no subscription required. You can also create your own song with a beat-synced video for $0.99, or a full cinematic lip-synced video starting at $2.99.
Can I create my own AI song?
Yes. Star Singer lets you create AI-generated songs and music videos. Clone your voice, pick any style, and generate original music. Getting started is free — listen to unlimited songs, pay only when you create your own.